Tuesday, 26 May 2015

UPENDO NA MAPENZI KATIKA NDOA.

  • Upendo na mapenzi katika ndoa ni mambo yanayoenda pamoja na havitakiwi viachane.,Upendo na mapenzi katika ndoa kila kimoja kina nafasi yake.,Kwanza kabisa katika ndoa upendo ni jambo la kwanza muhimu kuwepo.,Ili wanandoa waweze kwenda sawa ni lazima kuwepo na upendo wa dhati katika ndoa kwani upendo huvumilia,husamee,hautafuti mambo yake,husikilizana,huwa na kauli nzuri,unatia moyo katika maisha,hufadhili,kuambatana pamoja na mwenzio,hujali,haufurahii mabaya,haukinai na upo tayari kutia moyo.Mnaweza kuwa wanandoa lakini pasiwe na upendo wa kweli katikati yenu.Mapenzi huwa yanatawaliwa na tamaa kwani mtu anaweza akaoa/kuolewa na mtu asiyempenda ila kwa sababu ya fedha kalazimishwa,tamaa ya mwili na mali akafunga nae ndoa.,Ndoa yoyote isiyo na upendo ni vigumu kudumu na kuwepo kwa uaminifu kwa wana ndoa.

0 comments:

Post a Comment