Tuesday, 26 May 2015

MOYO WA MWANADAMU.

  • Kuna kipindi fulani mwanadamu hufikia uamuzi wa kumtafuta mwenzi wa maisha yake.,Kipindi hiki ndani ya moyo wake huwa mweupe hauna kitu,na kitu pekee anachokitafuta ni mtu ambaye atakayemfaa na kumkabidhi moyo wake.,Kipindi hiki huwa kigumu sana kwake,kama atakuwa mwanaume basi atakuwa na marafiki wengi wa kike na kama mwanamke atakuwa na marafiki wengi wa kiume,kipindi hiki moyo wake huangalia kuweza kupata mtu wa kushikamana nae kwa hiyo macho yake upapasa ili kumpata mtu aliye sahii huku moyo ukisubiri maamuzi ya macho ili uweze kupokea.,Wakati macho yakiangalia huku na uko ili kumpata aliye sahii huku ndani napo moyo huzungumza na macho kubaini aliye ashii,wakati macho yanatafuta ili kumpata aliye sahii ili yaweze kumkabidhi moyo utaona moyo nao unatamani.,Wakati macho yanatafuta kila kona kumpata aliye sahii ili yaweze kumkabidhi moyo,moyo nao huenda mbio kumpata aliye sahii wakati macho yanasema ni huyu nimempata moyo nao unakataa ya kwamba siyo huyo yaani hii inakuwa kama kuna mvutano kwani kazi ya macho ni kuona na kazi ya moyo ni kupokea.,Ni busara kufata maamuzi ya moyo na sio macho kwani macho hutamani kila unachokiona.

0 comments:

Post a Comment