Tuesday, 26 May 2015

KWENYE MAISHA.

  • Kwenye maisha kuna leo na kesho.,kwenye maisha kuna changamoto.,kwenye maisha kuna raha.,kwenye maisha kuna shida.,kwenye maisha kuna kupata na kukosa.,Haya yote unabudi huyatambue ili uweze songa mbele.,Ukiyajua haya uta teteleka utasimama imara kwa lolote litakalo kufika.

UPENDO NA MAPENZI KATIKA NDOA.

  • Upendo na mapenzi katika ndoa ni mambo yanayoenda pamoja na havitakiwi viachane.,Upendo na mapenzi katika ndoa kila kimoja kina nafasi yake.,Kwanza kabisa katika ndoa upendo ni jambo la kwanza muhimu kuwepo.,Ili wanandoa waweze kwenda sawa ni lazima kuwepo na upendo wa dhati katika ndoa kwani upendo huvumilia,husamee,hautafuti mambo yake,husikilizana,huwa na kauli nzuri,unatia moyo katika maisha,hufadhili,kuambatana pamoja na mwenzio,hujali,haufurahii mabaya,haukinai na upo tayari kutia moyo.Mnaweza kuwa wanandoa lakini pasiwe na upendo wa kweli katikati yenu.Mapenzi huwa yanatawaliwa na tamaa kwani mtu anaweza akaoa/kuolewa na mtu asiyempenda ila kwa sababu ya fedha kalazimishwa,tamaa ya mwili na mali akafunga nae ndoa.,Ndoa yoyote isiyo na upendo ni vigumu kudumu na kuwepo kwa uaminifu kwa wana ndoa.

MOYO WA MWANADAMU.

  • Kuna kipindi fulani mwanadamu hufikia uamuzi wa kumtafuta mwenzi wa maisha yake.,Kipindi hiki ndani ya moyo wake huwa mweupe hauna kitu,na kitu pekee anachokitafuta ni mtu ambaye atakayemfaa na kumkabidhi moyo wake.,Kipindi hiki huwa kigumu sana kwake,kama atakuwa mwanaume basi atakuwa na marafiki wengi wa kike na kama mwanamke atakuwa na marafiki wengi wa kiume,kipindi hiki moyo wake huangalia kuweza kupata mtu wa kushikamana nae kwa hiyo macho yake upapasa ili kumpata mtu aliye sahii huku moyo ukisubiri maamuzi ya macho ili uweze kupokea.,Wakati macho yakiangalia huku na uko ili kumpata aliye sahii huku ndani napo moyo huzungumza na macho kubaini aliye ashii,wakati macho yanatafuta ili kumpata aliye sahii ili yaweze kumkabidhi moyo utaona moyo nao unatamani.,Wakati macho yanatafuta kila kona kumpata aliye sahii ili yaweze kumkabidhi moyo,moyo nao huenda mbio kumpata aliye sahii wakati macho yanasema ni huyu nimempata moyo nao unakataa ya kwamba siyo huyo yaani hii inakuwa kama kuna mvutano kwani kazi ya macho ni kuona na kazi ya moyo ni kupokea.,Ni busara kufata maamuzi ya moyo na sio macho kwani macho hutamani kila unachokiona.

YAELEWE MAISHA.

  • Ukiwa duniani unatakiwa uwe na uwezo wa kutambua aina mbalimbali za maisha wanayoishi watu.Si vyema ukawa mtu wa kulalamika au kulaumu ovyo mtu kwa sababu ya ugumu wa maisha unayopitia.Wahenga pia husema dunia ni shule,ni jambo la busara kufahamu kuna leo na kesho,na kuna kupata na kukosa.Unaweza kupata leo na kesho ukakosa,na unaweza ukapata kesho na leo ukakosa.Kadri MUNGU anavyokupa neema ya kuishi muda mrefu ndivyo unavyozidi kuyafahamu maisha jinsi yalivyo hapa duniani.