- Mauaji ya albino ni aibu kwa taifa,Tunachafua taifa kwa tamaa za wachache,Tunaliaibisha taifa lenye Amani duniani,Furaha,Upendo,Heshima busara duniani.,MAUAJI YA ALBINO NI AIBU KWA TAIFA.
- Mauaji ya albino ni aibu kwa taifa,Tushikamane pamoja tuwasake watu hawa,Tuwafikishe kwenye vyombo vya sheria sheria ngumu itolewe,MAUAJI YA ALBINO NI AIBU KWA TAIFA.
- Mauaji ya albino ni aibu kwa taifa,Tushikamane pamoja tutokomeze ukatili,Aibu kwa taifa letu leo hii duniani,MAUAJI YA ALBINO NI AIBU KWA TAIFA.
SHAIRI.
MAUAJI YA ALBINO.
0 comments:
Post a Comment