- Ashukuriwe mungu muumba vyote duniani,yeye ndiye kiongozi wetu sisi duniani,salamu sisi twazitoa sisi tupo duniani,pokea salamu zetu baba yetu watupenda.
- Pendo lako la amani furaha hakuna kwingine,mungu wetu watupenda kamwe hakuna mwingine,twashukuru mungu wetu asante wewe ni baba,pokea salamu zetu baba yetu watupenda.
- Pendo lako la moyoni Baba twalipokea,Baba twasema asante Baba yetu wa milele,salamu zikufikie huko uliko Baba yetu,Pokea salamu zetu baba yetu watupenda.
SHAIRI.
ASHUKURIWE MUNGU.
0 comments:
Post a Comment