Friday, 9 January 2015

TUIPENDE TANZANIA

Mwaka tunaanza upya,tudumishe uzalendo.
Tuipende tanzania,tudumishe uzalendo.

Mungu katupa amani,tuilinde amani.
Tuipende tanzania tudumishe uzalendo.

Mbuga nzuri tunazo, ardhi yenye rutuba.
Tuipende tanzania ,tudumishe uzalendo.

Tushikamane pamoja,tuilinde tanzania.
Tuipende tanzania,tudumishe uzalendo.

Bendera yetu nzuri,mfano mmoja duniani.
Tuipende tanzania,tudumishe uzalendo.

0 comments:

Post a Comment