PAKA NA TABIA ZAKE.
- Paka anayefugwa na binadamu ana ukubwa wa uzito wa kilogram nne na tano.
- Paka anatabia anazo fanana na wanyama wengine kama vile simba,chui na duma.
- Paka ana uwezo mkubwa wa kusikia sauti ya chini kuliko binadamu anavyoweza kusikia.
- Paka uwinda,lakini anapokutana na paka wenzake au wanyama wengine utumia lugha za mwili wake kwa hajili ya mawasiliano,kuunguruma kwa sauti ya kutetema na kulia kwa sauti.
- Paka wakubwa wana uzito wa kilogram kumi na moja.
- Paka wadogo wana uzito wa kilogram 1.36.
- Paka wengi uwa na kimo cha wastani cha sentimeta 23 hadi 35.
- Paka pia uwa na urefu kuanzia kichwa hadi mkia wa wastani wa sentimita 46.
- Paka jike uwa na mkia mfupi.
- Paka dume uwa na mkia mrefu unaofika wastani wa sentimita 30.
- Paka ana fanana uti wa mgongo na wanyama wengine walio katika kundi la mamalia.
- Paka sehemu kubwa la fuvu lake limebeba macho,mataya magumu yenye nguvu na meno makari kwa hajili ya kuulia wanyama wadogo wadogo na kukatia nyama.
- Paka mwenye afya njema anao uwezo wa kufanya kazi wakati wowote usiku na mchana,ingawa wanaonekana kufanya kazi vizuri zaidi wakati wa usiku kuliko mchana.
- Paka kwa siku moja ana uwezo wa kuzunguka katika eneo la ukubwa la hekta 28 sawa na ekari 69 kwa siku.,ingawa muda wake mwingi uhutumia akiwa ametulia nyumbani.
- Paka wanaifadhi nguvu za miili yao kwa kusinzia.
- Paka ni mnyama mwenye usingizi mwingi kuliko wanyama wengine wa kundi lake na hata wasio wa kundi lake.
- Paka utumia saa 12 hadi 16 kwa siku akiwa amelala ambapo kwa paka wengine muda wa kulala kwa siku ni wastani wa saa 13 hadi 14,ingawa kuna baadhi ya paka wanaotumia hadi saa 20 kwa siku yenye saa 24 wakiwa usingizini.
0 comments:
Post a Comment