TABIA ZA PUNDA.
- Punda hutumika katika shughuli za kibinaadam, ubebaji maji, mizigo, kuvuta mikokoteni na pia katika kilimo.
- Punda ana wastani wa kimo cha sentimeta 80 mpaka 160.
- Punda anakadiliwa kuwa na uzito wa kilogramu 80 mpaka 450.
- Punda jike hujulikana kitaalamu kwa jina la Jenny.
- Punda dume hujilikana kitaalamu kwa jina la Jack.
- Punda pia hutoa kitoweo cha nyama.
- Punda jike hubeba mimba kwa kipindi cha miezi 12.
- Punda huzaa mtoto mmoja kwa kawaida kwa kila uzazi mmoja ila kuna wakati hutokea huzaa watoto mapacha.
- Punda mtoto wake mdogo wa kiume huitwa Colt.
- Punda mtoto wake mdogo wa kike huitwa Filly.
- Punda ana uwezo wa kuishi sehemu kame kwa muda mrefu kama vile jangwani na pia kukaa muda mrefu bila kunywa maji.
0 comments:
Post a Comment