- Mbio za mwanadamu duniani ni kujitafutia maitaji yake yaliyo sahii ili awezekuendelea kuishi hapa duniani,mpaka atakapo twaliwa ndipo itakuwa mwisho wa mbio zake hapa duniani.,Mbio za mwanadamu ni ndefu kwa maana anakimbia bila ya kuona mbele atafika lini.,Ni safari yenye kuitaji moyo jasiri ili uweze kuikamilisha ukiwa sawa,ni safari iliyojuu ya mambo mengi kuna kila aina ya vikwazo mbele yake,ila una budi uvishinde ili uweze kuimaliza safari yako salama,yenye amani,upendo na furaha kwako nakwa utakao waacha hapa duniani,watakukumbuka kwa yote uliyoyafanya hapa diniani na kuyaona kwa macho yao,watakukumbuka ucheshi wako,upole na unyeyekevu,ukari na upendo wako wataukumbuka sana kila mmoja atakumbuka kwako kitu kimoja kilichokuwa kinamfuraisha,mwengine upendo,mwengine ukari,mwengine upole na mwingine unyenyekevu,haya yote yatakuwa kumbukumbu toka kwako uliyowaachia,uwezi ukawaridhisha wanadamu wote ila kila mmoja utamridhisha kwa kile ulichokuwa nacho,na hata wasiyokupenda pia lazima utakuwa umewagusa kwa kitu kimoja bila ya wao wenyewe kujitambua ila siku ya mwisho kitajionesha miyoyoni mwao bila ya kujificha.,Hakika safari ya mwanadamu ni ndefu hinaitaji uvumilivu mkubwa ili aweze fika.,UVUMILIVU NI NINI ? Uvumilivu ni roho.,kila mwanadamu anazaliwa na uvumilivu ndani yake,ila kadri anavyokuwa mkubwa na kuweza kukumbana na mambo mengi ya dunia hii basi ujikuta akitoka katika hari hiyo ya uvumilivu na kujikuta akijiingiza katika hari ya kiarifu isiyotena na uvumilivu ndipo utamuona mtu ana kaba,ana uwa,ana baka,mwizi na mambo mengine mengi mabaya,roho ya uvumilivu inakuwa imekwisha toweka ndani yake,kuirudisha tena mpaka amrudie mungu.
MBIO ZA MWANADAMU.
MBIO ZA MWANADAMU DUNIANI.
0 comments:
Post a Comment