TABIA ZA KICHECHE.
- Kicheche ni mnyama anayepatikana katika bara la Afrika pekee hasa katika ukanda wa kisavana, isipokuwa kwenye misitu mikubwa ya Congo na baadhi ya maeneo ya Afrika magharibi ambako mnyama huyu hawezi kupatikana.
- Kicheche hapa nyumbani Tanzania anapatikana maeneo mengi hasa ya vijijini kwa umahiri wake wa kukamata kuku kwa njia ya ajabu.
- Kicheche ni mnyama jamii ya paka anayeishi porini ambaye kwa lugha ya kiingreza anaitwa "Zorilla" au "Polecat".
- Kicheche yupo kwenye kundi la mamalia, yupo kwenye familia ijulikanayo kama "Mustelidae" au "Weasels".
- Kicheche kama walivyo wanyama wengine wa jamii ya paka, pia yupo katika kundi la wanyama wanaokula nyama ambao kwa lugha ya kitaalamu wanaitwa "Carnivorous".
- Kicheche aliyekomaa ana urefu wa sentimeta 60 tu; sawa na futi mbili, urefu ambao unajumlisha mwili na mkia, mkia pekee una urefu wa sentimeta 20.
- Kicheche ni mnyama mwenye umbile dogo ila ana mbinu lukuki za kujiamini na maadui zake.
- Kicheche mbinu yake moja ya kujiamini na maadui zake ni kutoa harufu mbaya inayowaudhi maadui na hivyo badala ya adui kumdhuru huamua kumkimbia.
- Kicheche harufu mbaya anayoitoa huzalishwa kama kimiminika kwenye matezi maalum yaliyo kwenye sehemu yake ya kutolea haja kubwa.
- Kicheche kutokana na kutoa harufu mbaya nchini Sudan inadaiwa kumuita jina la "Father of stinks" yaan baba wa harufu mbaya.
- Kicheche ana tabia ya kuinua mkia wake kubinua mgongo ili aonekane mkubwa pindi anapokutana na adui yake ili amtishe.
- Kicheche ni mnyama mbinafsi wenyewe kwa wenyewe hawana tabia ya kushirikiana kwa jambo lolote isopokuwa wanapohitaji kushirikiana.
0 comments:
Post a Comment