Monday, 23 February 2015

SHAIRI.

MAUAJI YA ALBINO.
  • Mauaji ya albino ni aibu kwa taifa,Tunachafua taifa kwa tamaa za wachache,Tunaliaibisha taifa lenye Amani duniani,Furaha,Upendo,Heshima busara duniani.,MAUAJI YA ALBINO NI AIBU KWA TAIFA.
  • Mauaji ya albino ni aibu kwa taifa,Tushikamane pamoja tuwasake watu hawa,Tuwafikishe kwenye vyombo vya sheria sheria ngumu itolewe,MAUAJI YA ALBINO NI AIBU KWA TAIFA.
  • Mauaji ya albino ni aibu kwa taifa,Tushikamane pamoja tutokomeze ukatili,Aibu kwa taifa letu leo hii duniani,MAUAJI YA ALBINO NI AIBU KWA TAIFA.

Wednesday, 11 February 2015

SHAIRI.

ASHUKURIWE MUNGU.
  1. Ashukuriwe mungu muumba vyote duniani,yeye ndiye kiongozi wetu sisi duniani,salamu sisi twazitoa sisi tupo duniani,pokea salamu zetu baba yetu watupenda.
  2. Pendo lako la amani furaha hakuna kwingine,mungu wetu watupenda kamwe hakuna mwingine,twashukuru mungu wetu asante wewe ni baba,pokea salamu zetu baba yetu watupenda.
  3. Pendo lako la moyoni Baba twalipokea,Baba twasema asante Baba yetu wa milele,salamu zikufikie huko uliko Baba yetu,Pokea salamu zetu baba yetu watupenda.